31 Esau vilevile akatengeneza chakula kitamu, akamupelekea baba yake, akamwambia: “Basi baba, amuka ukule nyama ya mawindo yangu mimi mwana wako, upate kunibariki!”
Basi, Yakobo akakwenda kutwaa wana-mbuzi wawili na kuwaletea kwa mama yake. Naye akatayarisha chakula kitamu sawa vile baba yake Isaka alivyopenda.
Yakobo akamujibu baba yake: “Ni mimi Esau, muzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniagiza. Tafazali baba, amuka uikae ukule nyama ya mawindo yangu kusudi upate kunibariki.”
Isaka alipokwisha kumubariki Yakobo, naye Yakobo alipokuwa angali tu anatoka mbele ya baba yake Isaka, Esau kaka ya Yakobo, akarudi kutoka katika mawindo.
Halafu unitengenezee chakula kitamu, kile ninachopenda, uniletee nikule, nipate kukubariki mbele ya kufa kwangu.”