17 Basi, Isaka akaondoka kule, akapiga kambi yake katika bonde la Gerari, akakaa kule.
Halafu Abimeleki akamwambia Isaka: “Ondoka kwetu, maana wewe umetuzidi nguvu.”
Isaka akachimba vile visima vilivyokuwa vimechimbwa wakati Abrahamu baba yake alipokuwa muzima, visima ambavyo Wafilistini walikuwa wameziba nyuma ya kifo cha Abrahamu. Akavipa majina yaleyale baba yake aliyovipa.