Rebeka akamwambia Isaka: “Sina raha kabisa katika maisha kwa sababu ya hawa wanawake Wahiti wa Esau. Ikiwa Yakobo ataoa mumoja wa wanawake hawa Wahiti, maisha yangu yana faida gani?”
kule Makipela, upande wa mashariki wa Mamure, katika inchi ya Kanana. Abrahamu alinunua pango na shamba hilo kwa Efuroni, Muhiti, likuwe lake la kuzikia.
Daudi akamwambia Ahimeleki ambaye alikuwa Muhiti, na Abisai ndugu ya Yoabu (mama yao aliitwa Zeruya): “Nani atakwenda pamoja nami kwenye kambi ya Saulo?” Abisai akamwambia: “Mimi nitakwenda pamoja nawe.”