Isaka akachimba vile visima vilivyokuwa vimechimbwa wakati Abrahamu baba yake alipokuwa muzima, visima ambavyo Wafilistini walikuwa wameziba nyuma ya kifo cha Abrahamu. Akavipa majina yaleyale baba yake aliyovipa.
Lundo hili na nguzo hii ni ushuhuda kwamba mimi sitaruka lundo hili kuja kwako kukuzuru, wala wewe hautavuka lundo hili na nguzo hii kuja kwangu kunizuru.
Halafu akawaambia watu wote: “Jiwe hili ndilo litakalokuwa ushuhuda kwetu, maana limesikia maneno yote ambayo Yawe ametuambia. Kwa hiyo, litashuhudia juu yenu, kusudi musipate kumwasi Mungu wenu.”