26 Abimeleki akamwambia: “Mimi sijui nani aliyefanya hivyo. Mpaka leo hii wewe haukuniambia, wala mimi sijapata kusikia habari hizi mpaka leo.”
Basi, kukatokea ugomvi kati ya wachungaji wa Abramu na wachungaji wa Loti. Wakati ule, Wakanana na Waperizi ndio waliokuwa wenyeji wa inchi hiyo.
Wakati ule Abrahamu alikuwa amemwonya Abimeleki juu ya kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikuwa wamemunyanganya.
Basi, Abrahamu akatwaa kondoo na ngombe akamupa Abimeleki nao wawili wakafanya agano kati yao.