Kisha Abrahamu akamutahiri mwana wake Isimaeli, na kuwatahiri watumwa wanaume wote waliozaliwa katika nyumba yake na walionunuliwa kwa feza zake. Aliwatahiri wote siku hiyohiyo kama vile Mungu alivyomwamuru.
Nimemuchagua yeye na wazao wake. Yeye atawafundisha wazao wake kushika njia yangu kwa kutenda kwa haki na kwa kufuata sheria yangu, nami nitawatimizia ahadi zangu.”