Ukamwona kuwa wa haki mbele yako; ukafanya agano naye kuwapa wazao wake inchi ya Wakanana, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wayebusi na Wagirgasi. Na ahadi yako ukaitimiza; maana wewe ni mwaminifu.
Nyuma ya pale alitahiriwa, na kutahiriwa kwake kulikuwa kitambulisho cha kuhakikisha ile haki Mungu aliyomuhesabia kwa njia ya imani yake. Hivi Abrahamu akakuwa baba wa watu wote wanaoamini, ijapokuwa hawatahiriwi, kusudi wao vilevile wahesabiwe haki.
Uheri huu si kwa watu wanaotahiriwa tu, lakini ni kwa watu wasiotahiriwa vilevile. Kwa maana tumekwisha kusema kwamba Abrahamu alihesabiwa kuwa mwenye haki kwa njia ya imani yake.
Ndiyo kusema, Mungu ndiye aliyekuwa akipatanisha watu wote na yeye mwenyewe kwa njia ya Kristo bila kuhesabu makosa yao. Yeye ametupatia ujumbe wa upatanisho.
Kwa njia ya imani, Abrahamu alitii wakati Mungu alipomwita na kwenda katika inchi ile Mungu aliyoahidi kumupatia kuwa urizi wake. Akaacha inchi yake pasipo kujua pahali anapokwenda.