Kisha Daudi akamujengea Yawe mazabahu pahali pale na kumutolea sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani. Akamwomba Yawe, naye akakubali maombi yake kwa kuleta moto kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka kwenye mazabahu.
Mulima wa Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi kwa sababu Yawe alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto ule ulipanda juu kama moshi wa furu kubwa na mulima wote ukatetemeka kwa nguvu.
Watu waliposikia ngurumo na kuona umeme ukiwaka na kusikia sauti ya baragumu juu ya mulima uliokuwa unafuka moshi, wote wakaogopa na kutetemeka. Wote wakasimama mbali,
Hili ni agano nililowaagiza babu zenu kutii nilipowaondoa katika inchi ya Misri, kutoka katika shimo la moto. Niliwaambia wanitii na kufanya yote niliyowaamuru, na kwamba wakifanya hivyo, watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Basi wakati Manoa na muke wake walipokuwa wanaangalia ndimi za moto zikipanda juu mbinguni kutoka kwenye mazabahu, wakamwona malaika katika ndimi hizo akipanda kwenda mbinguni. Basi Manoa na muke wake wakainama uso mpaka chini.
Malaika wa Yawe akanyoosha fimbo yake, akagusa nyama na mikate kwa incha ya fimbo. Kwa rafla, moto ukatoka ndani ya jiwe, ukateketeza nyama na mikate. Mara moja malaika wa Yawe akatoweka mbele yake.