10 Hawa ndio wazao wa Semu. Miaka miwili nyuma ya yale mafuriko ya maji, Semu akiwa na umri wa miaka mia moja, alizaa Aripakisadi.
Nyuma ya kuzaa Aripakisadi, Semu aliishi miaka mia tano, na kupata wana wengine na wabinti.
Hawa ndio wazao wa Tera, baba ya Abramu, Nahori na Harani. Harani alikuwa baba ya Loti.