Ujumbe wa Mungu juu ya Tiro. Muomboleze, enyi mashua makubwa za kutoka Tarsisi. Kivuko na muji wenu vimeharibiwa. Mutapokea habari hizo mutakaporudia kutoka Kipuro.
Watu wa Tarsisi walifanya biashara nawe kwa sababu ya utajiri wako mwingi na wa kila namna. Walitoa feza, chuma, bati, na risasi kwa kupata biashara yako.
Walitwaa miti ya mialo toka Basani wakakuchongea makasia; walikutengenezea mbao za kuikalia kwa miti ya misunobari ya kisanga cha Kipuro, na kuipamba kwa pembe ya tembo.
Kitani kilichopindwa vizuri kutoka Misri kilikuwa kwa kupamba tanga lako na kwa ajili ya bendera yako. Chandarua chako kilitengenezwa na nguo ya rangi ya samawi na nyekundu-nyeusi kutoka visanga vya Elisa.
Mashua kutoka Kitimu zitamushambulia, naye atashikwa na hofu. Kisha atarudi nyuma akiwa amejaa hasira na kuvunja agano takatifu. Halafu atafuata shauri la wale walioasi agano takatifu.