Pandisha bendera ya vita katika dunia, piga baragumu kati ya mataifa; uyatayarishe mataifa kwa kupigana naye; uziite falme kwa kuishambulia; falme za Ararati, Mini na Askenazi. Weka jemadari juu yake; ulete farasi kama makundi ya nzige.
Vilevile makundi ya waaskari kutoka Gomeri, Beti Torgama, upande wa kaskazini kabisa, na makundi yao yote pamoja na makundi kutoka katika mataifa mengine, yako pamoja nawe.