Hawataelekea tena mazabahu ambazo ni kazi za vidole vyao wenyewe, wala kuzitazamia tena kazi za mikono yao wenyewe, ni kusema sanamu za mungu Ashera na mazabahu za kufukizia ubani.
Hivi ndivyo uovu wa wazao wa Yakobo utakavyoondolewa, hivi ndivyo zambi yake itakavyofutwa kabisa: ataziharibu mazabahu za miungu; mawe yake yatasagwasagwa kama chokaa. Sanamu za Ashera wala mazabahu za kufukizia ubani hazitabaki.
Yawe ameharibu bila huruma makao yote ya wazao wa Yakobo. Kwa kasirani yake amevibomoa vikingio vya watu wa Yuda. Ametupa chini na kuchafua ufalme wao na watawala wake.
Yawe ameamuru hivi juu ya Ninawe: Hautapata wazao kwa kulidumisha jina lako. Sanamu zako za kuchonga na za chuma chenye kuyeyushwa, nitazivunjavunja katika nyumba za miungu yako. Mimi nitakuchimbia kaburi lako, maana wewe haufai kwa kitu chochote.