Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Mika 5:13 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

13 Nitaziongoa sanamu za Ashera kutoka kwenu, na kuiangamiza miji yenu.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Mika 5:13
17 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Inchi yao imejaa sanamu za miungu, watu wake wanaabudu kazi ya mikono yao, vitu walivyotengeneza wao wenyewe.


Hivi ndivyo uovu wa wazao wa Yakobo utakavyoondolewa, hivi ndivyo zambi yake itakavyofutwa kabisa: ataziharibu mazabahu za miungu; mawe yake yatasagwasagwa kama chokaa. Sanamu za Ashera wala mazabahu za kufukizia ubani hazitabaki.


Nyumba zako wataziteketeza kwa moto na kuwafanya wanawake wengi waone azabu yako. Utakoma kujitoa kwa mutu yeyote afanye uzinzi nawe.


Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mutakuwa safi. Nitawatakasa toka uchafu wenu wote na toka uchafu wa sanamu za miungu yenu yote.


Hawatajichafua tena kwa kuabudu sanamu za miungu yao na kwa mambo yao ya kuchukiza wala kwa makosa yao. Nitawaokoa wasikuwe tena waasi. Nao watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.


Halafu wale walioponyoka watanikumbuka katikati ya mataifa ambamo watakuwa wamepelekwa katika uhamisho. Nitakuwa nimewavunja moyo wao wa uzinzi ambao ulinitupilia mbali, na macho yao yaliyozini na sanamu zao. Kwa hiyo watajichukia wao wenyewe kwa sababu ya maovu na machukizo yao yote waliyoyatenda.


Mioyo yao imejaa udanganyifu. Sasa ni lazima wabebe makosa yao. Yawe atabomoa mazabahu zao na kuziharibu nguzo zao.


Muombe huruma kwake, mumurudilie na kumwambia: Utusamehe uovu wote, upokee zawadi zetu, nasi tutakusifu kwa moyo.


Watarudi na kuishi chini ya ulinzi wangu, watastawi kama bustani nzuri. Watachanua kama muzabibu, harufu yao nzuri kama ya divai ya Lebanoni.


Yawe ameamuru hivi juu ya Ninawe: Hautapata wazao kwa kulidumisha jina lako. Sanamu zako za kuchonga na za chuma chenye kuyeyushwa, nitazivunjavunja katika nyumba za miungu yako. Mimi nitakuchimbia kaburi lako, maana wewe haufai kwa kitu chochote.


Nitaunyoosha mukono wangu kwa kuazibu inchi ya Yuda, pamoja na wakaaji wote wa Yerusalema. Nitaangamiza mabaki yote ya mungu Bali kutoka inchi hii, na hakuna atakayetambua jina lao.


Wakati ule, nitaondoa majina ya sanamu za miungu katika inchi, wala hayatakumbukwa tena. –Ni ujumbe wa Yawe wa majeshi.– Na wanaojidai kuwa manabii nitawaondoa kabisa pamoja na tamaa zao za kuabudu sanamu.


Watu waliobaki bila kuuawa na yale mapigo hawakuachana na sanamu walizojitengenezea wao wenyewe. Hawakuacha kuabudu pepo, sanamu za zahabu, za feza, za shaba, za mawe na za miti zisizoweza kuona, wala kusikia, wala kutembea.


Wale watu watano waliokwenda kuipeleleza inchi wakaingia ndani, wakabeba ile sanamu ya mungu yenye kuyeyushwa, kile kizibao na sanamu ya ibada. Wakati ule yule kuhani alikuwa akisimama kwenye mulango pamoja na wale watu mia sita wenye silaha.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ