Yawe anasema: Mimi ninafanya nanyi agano hili: Roho wangu anayekuwa juu yenu, maneno niliyoyaweka katika kinywa chenu, hayataondoka kwenu hata kidogo, wala kwa watoto na wajukuu wenu, tangu sasa na hata milele.
Zambi ya watu wa Yuda, haiwezi kufutikana, imeandikwa kwa kalamu ya chuma; kwa chongo ya almasi. Imechorwa ndani ya mioyo yao na kwenye pembe za mazabahu yao.
Kisha siku hizo, nitafanya agano hili na Waisraeli. Nitaiweka sheria yangu ndani yao, na kuiandika katika mioyo yao. Mimi nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Ni mimi Yawe ninayesema hivyo.
Inaonekana wazi kwamba ninyi ni barua iliyoandikwa na Kristo na kutumwa kwa njia ya utumishi wetu. Barua hii inaandikwa si kwa wino, lakini kwa Roho wa Mungu Mwenye Uzima. Barua hiyo haikuandikwa juu ya vibao vya mawe, lakini katika mioyo ya watu.