Anayetaka kujivuna, ajivune kwamba ananifahamu mimi, kwamba anajua kwamba mimi Yawe ninatenda mema, ninafanya mambo ya haki kufuatana na sheria yangu katika dunia. Watu wa namna hiyo ndio wanaonipendeza. –Ni ujumbe wa Yawe.
Wakati mwingine wingu hilo lilikaa juu ya hema kwa muda wa siku chache tu. Kwa agizo la Yawe, Waisraeli walipiga kambi na ni kwa agizo la Yawe walisafiri.
Ikiwa ni siku mbili, mwezi, mwaka au zaidi, muda wote wingu hilo lilipokuwa juu ya hema, Waisraeli hawakuhama; lakini lilipoinuliwa, nao vilevile walihama.