Yawe amekulipiza kisasi kutokana na kumwanga damu ya watu wote wa jamaa ya Saulo, ambaye sasa wewe umenyanganya ufalme kwa pahali pake. Sasa, Yawe amemupa mwana wako Abusaloma ufalme. Maangamizi yamekupata kwa sababu wewe ni mwuaji.”
Kwa sababu watu wa Israeli, walipokuwa wanasafiri toka Misri, wao hawakuwapa chakula wala maji ya kunywa, pahali pake wakamulipa Balamu kwa kuwalaani watu wa Israeli, lakini Mungu wetu akageuza laana yao kuwa baraka.
Goliati akamwuliza Daudi: “Sasa, hiyo fimbo ni ya nini? Unazani mimi ni imbwa hata unifikie kwa fimbo?” Mufilistini yule akamulaani Daudi kwa miungu yake.