Palepale maneno yako yaliponifikia, niliyameza; nayo yakanifurahisha, yakakuwa matamu katika moyo wangu, maana mimi ninajulikana kwa jina lako, ee Yawe wa majeshi.
Ni kazi ya makuhani kuwafundisha watu maarifa ya kweli juu ya Mungu kusudi watu wawaendee kwa kujifunza mapenzi yangu kwao, maana makuhani ni wajumbe wa Yawe wa majeshi.