Musiseme neno lolote baya, lakini kama ni lazima museme tu maneno mazuri na ambayo yanasaidia kuwajenga wengine na yanayoleta neema kwa wale wanaoyasikia.
Nao ulimi ni kama moto. Ulimi ni kiungo kinachojaa ubaya wa kila namna. Ulimi unapatikana kwenye nafasi yake katikati ya viungo vyetu, nao ndio unaochafua mwili wote. Unateketeza maisha yetu ukichomwa wenyewe na moto unaotoka katika jehenamu.