Kisha, mufalme Daudi akamwambia Solomono mwana wake: “Uwe imara na hodari, ufanye kazi hii. Usiogope wala kuwa na wasiwasi. Yawe Mungu ambaye ni Mungu wangu, yuko pamoja nawe. Hatakuachilia lakini atakuwa nawe mpaka itakapomalizika kazi yote ambayo inayohitajika kufanyiwa kwa nyumba ya Yawe.
“Nawe Solomono mwana wangu, umujue Mungu wa baba yako, na umutumikie kwa moyo wako wote na kwa nia nzuri; yeye Yawe anachunguza mioyo na anafahamu mipango na mafikiri ya mwanadamu. Ukimutafuta yeye, utamwona; lakini ukimwacha, atakutupilia mbali milele.