Halafu wale walioponyoka watanikumbuka katikati ya mataifa ambamo watakuwa wamepelekwa katika uhamisho. Nitakuwa nimewavunja moyo wao wa uzinzi ambao ulinitupilia mbali, na macho yao yaliyozini na sanamu zao. Kwa hiyo watajichukia wao wenyewe kwa sababu ya maovu na machukizo yao yote waliyoyatenda.
Lakini watu wenye woga, wasioamini, wenye machukizo, wauaji, wazinzi, wachawi, wanaoabudu sanamu na wote wanaosema uongo, fungu lao ni katika lile ziwa la moto na ndani ya mawe ya kiberiti yanayowaka moto. Hiki ndicho kifo cha pili.”