Lakini ninyi mumepanda uovu, ninyi mumevuna ubaya; mumekula matunda ya uongo wenu. Wewe Israeli ulitegemea nguvu zako mwenyewe, na wingi wa waaskari wako.
Mateso uliyoyatenda kule Lebanoni yatakulemea wewe; uliwaua nyama, nyama nao watakuogopesha. Yote hayo yatakupata wewe, kwa mauaji na mateso uliyoitendea dunia, uliyoifanyia miji na wakaaji wake wote.
Wewe umenyanganya mataifa mengi, lakini wote wanaobaki watakunyanganya wewe, kwa mauaji na mateso uliyoitendea dunia, uliyoifanyia miji na wakaaji wake wote.