Ahitofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, alitandika punda wake, akaenda kwake, kwenye muji wake. Alipofika kule, alipanga vizuri mambo ya nyumba yake, akajitundika. Akakufa na kuzikwa kwenye kaburi la baba yake.
Halafu Waisraeli wakageuka kwa kupigana, na watu wa kabila la Benjamina wakashikwa na woga maana sasa waliona kwamba kuangamia kwao kulikuwa kumekaribia.