1 Mizani danganyifu ni chukizo kwa Yawe, lakini matumizi ya vipimo vya haki ni furaha kwake.
Mizani na vipimo vya kweli ni vya Yawe. Mawe yote ya kupimia katika mufuko ni kazi yake.
Mizani danganyifu na vipimo danganyifu, vyote ni chukizo kwa Yawe.
Mizani danganyifu ni chukizo kwa Yawe, na vipimo visivyokuwa vya haki ni kitu kibaya.
Lakini ninyi mumurudilie Mungu wenu. Mushikamane na wema na haki, mumutumainie Mungu wenu siku zote.
Efuraimu ni sawa na muchuuzi anayetumia vipimo vya udanganyifu, anayependa kudanganya watu.