Basi, nitawaletea taabu; zile hasara zote wanazoogopa zitawapata; maana nilipoita hakuna aliyeitika, niliposema hawakunisikiliza. Lakini walifanya maovu mbele yangu, walichagua yale ambayo hayanipendezi.
Na hao ambao waliowatabiria mambo hayo, maiti zao zitatupwa katika barabara za Yerusalema wakiuawa kwa njaa na vita, wala hakutakuwa mutu wa kuwazika wao wenyewe, wake zao, wabinti zao na wana wao. Mimi nitawabebesha lazima ya uovu wao wenyewe.
Uovu wako utakuazibu; na uasi wako utakuhukumu. Ujue na kutambua kwamba ni vibaya sana kuacha Bwana wako Yawe, Mungu wako, na kutokuwa na woga wangu ndani yako. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe wa majeshi.–
Sikiliza, ee dunia! Mimi nitawaletea watu hawa hasara kulingana na nia zao mbaya. Maana hawakuyajali maneno yangu, na mafundisho yangu nayo wameyakataa.