Yesu alianza kufundisha tena pembeni ya ziwa la Galilaya. Kundi kubwa la watu walikusanyika karibu naye, kwa hiyo akaingia ndani ya chombo na kuikaa mule. Chombo kilikuwa katika ziwa na watu walisimama inchi kavu, pembeni ya ziwa.
Yesu akashuka toka kilima pamoja na wanafunzi wake, na kusimama kwenye uwanja. Pale kulikuwa wanafunzi wake pamoja na kundi kubwa sana la watu waliotoka Yerusalema, katika Yudea yote na pande za miji Tiro na Sidona pembeni ya bahari.
Ilipotimia karibu siku nane nyuma ya pale Yesu aliposema maneno hayo, yeye akawatwaa Petro, Yakobo na Yoane, akapanda pamoja nao kwa mulima kwa kuomba.