Siku ya Sabato ilipokwisha kupita, kesho yake siku ya kwanza ya juma, kwa wakati wa mapambazuko, Maria wa Magdala na Maria mwingine wakaenda kuangalia kaburi.
pamoja na wanawake wamoja ambao alikuwa ameondosha pepo ndani yao na magonjwa mengine. Kati ya wale wanawake kulikuwa Maria (aliyeitwa wa Magdala), aliyekuwa ameponyeshwa pepo saba;
Siku ya kwanza ya juma asubui mapema, kulipokuwa kungali giza, Maria wa Magdala akaenda kwenye kaburi. Alipofika kule akaona kama jiwe lililofunika kaburi limeondolewa.