39 Watu waliokuwa wakipita pale walimutukana, na kutikisatikisa vichwa vyao,
Hili ndilo neno Yawe alilosema juu yake: “Watu wa Sayuni wanakuzarau kabisa, watu wa Yerusalema wanakutikisia kichwa kwa kukuchekelea.
Kama mungekuwa mimi, na mimi ninyi, ningeweza kusema kama ninyi. Ningeweza kutunga maneno juu yenu, na kutikisa kichwa changu.
Kwa maana Mungu ameniregeza na kunishusha, wamekuwa huru kunitendea wanavyopenda.
Watu waovu na wadanganyifu wananishambulia, wanasema uongo juu yangu.
Watu wananichekelea; wanaponiona wanatikisa vichwa vyao kwa kunizarau.
Kundi la waovu limenizunguka; wananizunguka kama kundi la imbwa; wamenitoboa mikono na miguu.
Wewe unajua ninavyotukanwa, unajua haya na matusi ninazopata; na waadui zangu wote wewe unawajua.
Enyi wapita njia wote, hivi hamujali kitu? Muangalie, muone kama kuna aliyepatwa na uchungu kama mimi, uchungu Yawe alioniletea siku ya hasira yake kali.
Vilevile wanyanganyi wawili walitundikwa juu ya misalaba pamoja na Yesu, mumoja kwa upande wake wa kuume na mwingine kwa upande wa kushoto.
Nao walimutusi kwa maneno mengine mengi.