Yesu alipokuwa akitembea pembeni ya ziwa la Galilaya, akawaona wavuvi wawili, waliokuwa wandugu wa tumbo, Simoni (aliyeitwa Petro) na ndugu yake Andrea. Walikuwa wakitupa nyavu katika ziwa.
Yesu alipoendelea mbele kidogo, akawaona wandugu wengine wawili, Yakobo na Yoane, waliokuwa wana wa Zebedayo. Walikuwa ndani ya chombo pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Yesu akawaita.
“Sasa roho yangu inafazaika. Nami sijui niseme nini. Nimwombe Baba, aniokoe toka mambo yale yatakayofika saa hii? Hapana, kwa sababu nimefika kwa ajili ya yale yatakayofanyika saa hii.