naye Petro akakumbuka maneno yale Yesu aliyomwambia kwamba mbele jogoo hajawika, atakuwa amemukana mara tatu. Basi akatoka inje, akalia kwa uchungu sana.
Mara moja jogoo akawika kwa mara ya pili, na Petro akakumbuka maneno yale Yesu aliyomwambia kwamba mbele jogoo hajawika mara mbili, atakuwa amemukana mara tatu. Basi akaanza kulia.
Yesu akamujibu: “Hakika wewe ni tayari kutoa maisha yako kwa ajili yangu? Kweli, kweli ninakuambia: mbele jogoo hajawika, utakuwa umekwisha kunikana mara tatu.”