Daudi akainua macho yake, akamwona yule malaika wa Yawe akisimama kati ya mbingu na dunia, naye akiinua upanga wake juu ya Yerusalema tayari kuangamiza. Halafu Daudi na wazee wote walikuwa wakivaa nguo ya gunia, wakaanguka uso mpaka chini.
Basi, nikasimama na kwenda katika bonde. Nikiwa huko nikauona utukufu wa Yawe ukiwa umesimama huko kama utukufu ule niliokuwa nimeuona karibu na muto Kebari; nami nikaanguka uso mpaka chini.
Maono hayo yalikuwa kama maono niliyoyaona wakati Mungu alipokuja kuuangamiza Yerusalema. Vilevile yalifanana na maono niliyoyaona karibu na muto Kebari. Nikaanguka uso mpaka chini.
Gabrieli akakuja karibu na pahali niliposimama. Mimi nikaogopa sana, hata nikaanguka uso mpaka chini. Lakini akaniambia: Wewe mutu, uelewe kwamba maono uliyoyaona yanaelekea wakati wa mwisho.
Yawe akawasha moto ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa na mafuta yaliyokuwa juu ya mazabahu. Watu wote walipoona huo moto wakapiga vigelegele na kuinama uso mpaka chini.
Sisi wote tukaanguka chini, na nikasikia sauti iliyoniambia hivi katika luga ya Kiebrania: ‘Saulo, Saulo, kwa sababu gani unanitesa? Unajiumiza bure kama ngombe anayepiga teke kwenye chongo ya fimbo ya mwenyeji wake.’
Basi wakati Manoa na muke wake walipokuwa wanaangalia ndimi za moto zikipanda juu mbinguni kutoka kwenye mazabahu, wakamwona malaika katika ndimi hizo akipanda kwenda mbinguni. Basi Manoa na muke wake wakainama uso mpaka chini.