na kuwapa wale wanaoomboleza katika Sayuni taji la maua pahali pa majivu juu ya kichwa, mafuta ya kuangarisha kwa furaha pahali pa maombolezo, nguo ya sifa pahali pa moyo muzito. Nao wataitwa miti ya mialo ya haki, Yawe aliyopanda kuonyesha utukufu wake.
Kufika kwao kunaleta machafuko katika karamu zenu za upendo. Wanakula na kushiba pamoja nanyi pasipo haya yoyote. Wao ni kama mawingu yanayopeperushwa na upepo pasipo kuleta mvua. Wao ni kama miti isiyozaa matunda hata wakati wa mavuno; ni miti iliyoongolewa na kufa kabisa.