12 Wanafunzi wa Yoane wakakuja kubeba maiti yake na kuizika. Nao wakaenda kumwelezea Yesu habari ile.
Halafu wakaleta kile kichwa chake ndani ya sahani na kukitoa kwa yule binti, naye akakipeleka kwa mama yake.
Yesu aliposikia habari hii, akaondoka pale ndani ya chombo, na kwenda peke yake kwa pahali penye ukiwa. Nayo makundi ya watu waliposikia vile, wakatoka katika miji yao na kumufuata Yesu kwa miguu.
Wakati wanafunzi wa Yoane walipopata habari ile, wakaenda kubeba maiti yake na kuizika.
Watu wenye kuogopa Mungu wakamuzika Stefano na kumufanyia kilio kikubwa.