Farasi wanaweza kukimbia katika mawe makubwa? Watu wanaweza kulima bahari na ngombe? Lakini ninyi mumeigeuza sheria kuwa sumu, na tunda la haki kuwa uchungu.
Wakaifanya mioyo yao kuwa migumu kama jiwe, wasipate kusikia sheria yangu mimi Yawe wa majeshi niliyoitangaza kwa roho yangu kwa kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyo, mimi Yawe wa majeshi nikawaka hasira juu yao,