Miaka mitatu mbele ya pale, Yawe alimwambia Isaya mwana wa Amozi hivi: Kwenda uvue nguo ya gunia uliyokuwa umevaa katika kiuno, na viatu vyako. Isaya akafanya kama alivyoambiwa; akakuwa anatembea uchi na bila viatu.
Wale wanafunzi wa Yoane walipoondoka, Yesu akaanza kuwaambia makundi ya watu habari za Yoane: “Mulienda katika jangwa kwa kuangalia nini? Tete linalotikiswa na upepo? Hapana!
Nimesumbuka kwa kufanya kazi ngumu, nimepata magumu, nimekesha mara nyingi. Mara nyingi niliteswa na njaa na kiu; mara nyingi nililazimishwa kutokula. Nimeteseka na baridi na ukosefu wa nguo.
Nami nitawatuma washuhuda wangu wawili, wakiwa wamevaa nguo za kilio. Nao watatangaza ujumbe wa Mungu kwa muda wa siku elfu moja mia mbili na makumi sita.”