Kisha kuwaamuru watu waikae juu ya majani, Yesu akatwaa ile mikate mitano na samaki mbili, akainua macho mbinguni, akamushukuru Mungu. Akamega ile mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakaigawanya kwa kundi la watu.
Basi Yesu akawaamuru watu waikae chini. Kisha akakamata ile mikate saba, akamushukuru Mungu, akaimega na kuwapa wanafunzi wake waigawanye kwa watu; nao wanafunzi wakaigawanya.