Siku moja, wakati wa mazishi, watu waliona moja kati ya makundi yale. Wakatupa maiti katika kaburi la Elisha na kukimbia. Mara tu maiti hiyo ilipogusa mifupa ya Elisha, ilifufuka na kusimama wima.
Na kila pahali Yesu alipokwenda, katika vijiji, miji, au kwenye mbuga, watu waliweka wagonjwa katika viwanja vya makutano na kumusihi awaache wagonjwa waguse hata upindo wa kanzu yake tu. Nao wote waliougusa, walipona.
Na kufuatana na mambo yote yaliyotokea, watu waliwapeleka wagonjwa katika barabara, wakiwalalisha juu ya mikeka na vipoyi kusudi Petro atakapopita, kivuli chake kipate tu kufika kwenye wamoja wao.