Yesu akawaruhusu. Halafu wale pepo wakatoka ndani ya mutu yule na kuingia ndani ya nguruwe. Kundi zima la nguruwe, karibu elfu mbili, wakatelemuka mbio kwenye mulima na kutumbukia ndani ya ziwa, nao wakazama ndani ya maji.
Walipomufikia Yesu, wakamwona yule aliyekuwa na kundi la pepo ndani yake akiikaa, akiwa amevaa nguo nayo akili yake ikiwa sawa. Basi watu wale wakaogopa.