Yesu alizunguka katika Galilaya yote akifundisha katika nyumba zao za kuabudia, akihubiri Habari Njema ya Ufalme. Aliponyesha watu waliokuwa na magonjwa yote na uzaifu wa kila namna.
Na kila pahali Yesu alipokwenda, katika vijiji, miji, au kwenye mbuga, watu waliweka wagonjwa katika viwanja vya makutano na kumusihi awaache wagonjwa waguse hata upindo wa kanzu yake tu. Nao wote waliougusa, walipona.
Yesu akaingia ndani ya moja kati ya vile vyombo, nacho kilikuwa cha Simoni. Yesu akamwomba akisukume mbali kidogo na kivuko. Halafu akaikaa mule na kuwafundisha watu.
Na kufuatana na mambo yote yaliyotokea, watu waliwapeleka wagonjwa katika barabara, wakiwalalisha juu ya mikeka na vipoyi kusudi Petro atakapopita, kivuli chake kipate tu kufika kwenye wamoja wao.