Kwa mwisho Yesu akawatokea wanafunzi kumi na mumoja walipokuwa wakikula. Naye akawakaripia kwa sababu ya kutokuamini kwao na kwa sababu ya ugumu wao. Kwa maana hawakusadikia wale waliomwona nyuma ya kufufuka kwake.
Wanafunzi wengine wakamwambia: “Tumemwona Bwana.” Lakini Toma akawajibu: “Nisipoona alama za misumari katika mikono yake na kutia kidole changu katika kovu za misumari ile, nami nisipoingiza vidole vyangu ndani ya ubavu wake, sitaamini.”