Wajane wao wamekuwa wengi kuliko muchanga wa bahari. Nao wamama wenye watoto vijana nimewaletea mwangamizaji muchana kati. Nimesababisha uchungu na vitisho viwapate kwa rafla.
Kwa hiyo uwaache watoto wao wakufe kwa njaa, uwaache wakufe kwa vita. Wake zao wakuwe tasa na wajane. Waume zao wakufe kwa magonjwa makali na vijana wao wachinjwe kwa upanga katika vita.