Pumzi yake ni kama mafuriko ya muto ambao maji yake yanafika mpaka kwenye shingo. Anakuja kupepeta mataifa kwa lungo ya maangamizi, kuwafunga lijamu na kuwapeleka wasikotaka.
Ee Yawe, mbona unatukosesha njia zako? Mbona unaifanya mioyo yetu kuwa migumu hata tusikuogope? Urudie, ee Mungu, kwa ajili ya watumishi wako, makabila ambayo yalikuwa mali yako siku zote.