Kisha Yawe akaniambia: Hata kama Musa na Samweli wangesimama mbele yangu na kunisihi, singewahurumia watu hawa. Uwaondoe kabisa mbele yangu. Uwaache waende!
Kwa hasira yake, Yawe amewaweka watu wa Sayuni katika giza. Ametupa toka mbinguni mpaka katika dunia utukufu wa Israeli. Kwa siku ya hasira yake, alilitupilia mbali hata hekalu lake.