Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efuraimu, kama simba mukali kwa watu wa Yuda. Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka, nitawakamata na hakuna atakayewaokoa.
Halafu watasema: Tuende tumurudilie Yawe! Yeye mwenyewe ameturarua, lakini yeye mwenyewe atatuponyosha. Yeye mwenyewe ametuumiza, lakini yeye mwenyewe atatunza vidonda.