Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Maombolezo 1:2 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

2 Unalia usiku kucha; machozi yanatiririka juu ya mashavu yake. Hakuna hata mumoja kati ya wapenzi wake kwa kuufariji. Rafiki zake wote wameudanganya; wamekuwa waadui zake.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Maombolezo 1:2
30 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Warafiki zangu wamenidanganya kama kijito, wamenidanganya kama mifereji isiyokuwa na maji,


Basi nimepangiwa miezi na miezi ya taabu, urizi wangu ni kuteseka usiku kwa usiku.


Wanaopanda kwa machozi, watavuna kwa shangwe.


Maisha yangu yamekwisha kwa ajili ya kuugua; nayo miaka yangu kwa ajili ya kusikitika. Nguvu zangu zimeniishia kwa kutaabika; hata mifupa yangu imekauka.


Huko kwa wafu hakuna anayekukumbuka; katika kuzimu ni nani anayeweza kukusifu?


Matusi yamevunja moyo wangu, nami nimekata tamaa. Nimetafuta kitulizo lakini sikupata, nimetafuta wa kunifariji lakini sikumupata.


Masikini anachukiwa na wandugu zake; warafiki zake ndio zaidi: wanamukimbia! Hata awabembeleze namna gani, hatawapata.


Na kama musiponisikiliza, moyo wangu utalia machozi kwenye uficho, kwa sababu ya kiburi chenu. Nitalia kwa uchungu na kutoa machozi, maana watu wa Yawe wanapelekwa katika uhamisho.


Israeli, usiichubue miguu yako wala usilikaushe koo lako. Lakini wewe unasema: Hakuna tumaini lolote. Ninapenda miungu ya kigeni, hiyo ndiyo nitakayoifuata.


Mume akiachana na muke wake, naye muke akijiendea, na kuolewa na mwingine, mume yule anaweza kumurudilia muke huyo? Kufanya hivyo hakutaichafua inchi kabisa? Wewe Israeli, umefanya ukahaba na wapenzi wengi, sasa unataka kunirudilia mimi? –Ni ujumbe wa Yawe.–


Wapenzi wako wote wamekusahau; hawajali kitu chochote juu yako. Nimekupiga sawa vile ungekuwa adui yangu. Umeazibiwa bila huruma, kwa sababu kosa lako ni kubwa, zambi zako ni nyingi sana.


Nawe Yerusalema uliyeachwa tupu, kwa nini sasa unavaa nguo nzuri nyekundu? Kwa nini kujipamba kwa zahabu, na kujipakaa wanja kwenye macho? Unajipamba bure! Wapenzi wako wanakuzarau sana; wanatafuta kukuua tu.


Heri ningepata kibanda cha wasafiri katika jangwa, ningewaacha watu wangu na kujiendea. Wote ni wazinzi, ni kundi la watu waasi.


Niliwaita wapenzi wangu, lakini wao wakanidanganya. Makuhani na wazee wangu wamekufia katika muji, wakijitafutia chakula kusudi wajirudishie nguvu zao.


Sikiliza ninavyolalamika; hakuna wa kunifariji. Waadui zangu wote wamesikia juu ya taabu yangu: wanafurahi kwamba umeniletea hasara. Uifanye ile siku uliyoahidi ifike, uwafanye nao wateseke kama mimi.


Uchafu wake ulionekana waziwazi, lakini muji wenyewe haukujali mwisho wake. Anguko lake lilikuwa kubwa sana; hakuna anayeweza kuufariji. Unasema: Angalia, ee Yawe, mateso yangu, maana adui yangu ameshinda.


Macho yangu yamevimba kwa kulia, roho yangu imechafuka, moyo wangu una huzuni nyingi, kwa sababu ya kuangamizwa kwa watu wangu, kwa sababu watoto wachanga na wale wanaonyonya wanazimia katika barabara za muji.


Basi, mimi nitawakusanya wapenzi wako wote uliojifurahisha nao, wote uliowapenda na wote uliowachukia. Nitawakusanya toka pande zote wakushambulie. Nitawafunulia uchi wako wapate kuuona.


Mama yao amefanya uzinzi, aliyebeba mimba yao amefanya mambo ya haya. Alisema: Nitaambatana na wapenzi wangu, ambao wananipatia chakula na maji, nguo za sufu na kitani, pamoja na mafuta na divai.


Usimwaminie mwenzako, wala usimutumainie rafiki yako. Chunga mudomo wako, usimwambie kitu muke wako wewe mwenyewe.


Hawa wote kumi wako na shabaha moja ya kumupa yule nyama uwezo wao na mamlaka yao.


Zile pembe kumi ulizoona na yule nyama wa ajabu watamuchukia yule kahaba. Watamunyanganya vyote anavyokuwa navyo na kumwacha uchi. Nao watakula nyama ya mwili wake na kuteketeza mabaki yake kwa moto.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ