Nilitaka kuchuma matunda kutoka kwao. –Ni ujumbe wa Yawe.– Lakini sikupata zabibu hata moja juu ya muzabibu, sikupata tini zozote juu ya muti wa tini; hata majani yao yamekauka. Hata nilichokuwa nimewapa kimetoweka.
Nzige, makundi kwa makundi, wameishambulia mimea; kilichoachwa na nzige kimekuliwa na tunutu, kilichoachwa na tunutu kimekuliwa na parare, kilichoachwa na parare kimeliwa na panzi.
Nitawaondoa hao waadui wanaotoka kaskazini, nitawafukuza mpaka katika jangwa; waaskari wa mbele nitawatupa katika bahari ya Chumvi na wale wa nyuma katika bahari ya Mediteranea. Watatoa uvundo na harufu mbaya, hao ambao wamefanya maovu makubwa.
Niliwapiga pigo la ukosefu wa maji na ukungu; nikakausha bustani na mashamba yenu ya mizabibu; nzige wakakula miti ya tini na mizeituni yenu. Hata hivyo hamukunirudilia. –Ni ujumbe wa Yawe.–
Hata kama miti ya tini isipochanua maua wala mizabibu kuzaa zabibu, hata kama mizeituni isipozaa zeituni na mashamba yasipotoa chakula, hata kama kondoo wakitoweka katika zizi na nyama wa kufugwa kukosekana katika mazizi,
Nimeleta ukavu katika inchi, juu ya vilima na mashamba ya ngano, mashamba ya mizabibu na mashamba ya mizeituni na kila mumea, watu na nyama, na chochote mulichokitoshea jasho. –Ni ujumbe wa Yawe wa majeshi.
Mimea yenu yote muliyojaribu kupanda, niliiharibu kwa kuikausha na kwa kuipiga kwa ukungu na mvua ya mawe, lakini hata hivyo hamukunirudilia. –Ni ujumbe wa Yawe.–
Sasa nitaleta tena amani katika dunia, mvua itanyesha kama kawaida, udongo utatoa mazao, na mizabibu itazaa kwa wingi. Nitawapa watu wanaobaki wa taifa hili yale yote yakuwe mali yao.