15 Nao wanafunzi wakafanya vile, wakawaikalisha watu wote.
(Watu waliokuwa pale walikuwa yapata wanaume elfu tano.) Yesu akawaamuru wanafunzi wake wawaikalishe kwa makundi ya watu makumi tano tano.
Kisha Yesu akatwaa ile mikate mitano na samaki mbili, akainua macho mbinguni, akamushukuru Mungu. Halafu akaimega, akawapa wanafunzi waigawanyie watu.