Basi Yesu akawaamuru watu waikae chini. Kisha akakamata ile mikate saba, akamushukuru Mungu, akaimega na kuwapa wanafunzi wake waigawanye kwa watu; nao wanafunzi wakaigawanya.
Lakini Yesu akawajibu: “Ninyi wenyewe muwape chakula!” Nao wakajibu: “Sisi tuko tu na mikate mitano na samaki mbili. Unataka sisi wenyewe tuende kuwanunulia watu hawa wote chakula?”