Siku moja, wakati wa mazishi, watu waliona moja kati ya makundi yale. Wakatupa maiti katika kaburi la Elisha na kukimbia. Mara tu maiti hiyo ilipogusa mifupa ya Elisha, ilifufuka na kusimama wima.
Na kila pahali Yesu alipokwenda, katika vijiji, miji, au kwenye mbuga, watu waliweka wagonjwa katika viwanja vya makutano na kumusihi awaache wagonjwa waguse hata upindo wa kanzu yake tu. Nao wote waliougusa, walipona.
Siku moja Yesu alipokuwa akifundisha, Wafarisayo na walimu wakubwa wa Sheria waliotoka katika kila kijiji cha jimbo la Galilaya na la Yudea na toka Yerusalema, walikuwa wakiikaa pale. Naye alikuwa akiponyesha wagonjwa kwa uwezo wa Bwana.
Lakini ninyi ni watu wa kizazi kilichochaguliwa na Mungu na wa ukuhani wa kifalme. Ninyi ni taifa takatifu na watu wa pekee wa Mungu. Mumechaguliwa kusudi mutangaze matendo makubwa ya yule aliyewaita kutoka katika giza na kuwaingiza kwenye mwangaza wake wa ajabu.