Nitawaongoza vipofu katika njia wasiyoifahamu, nitawaongoza katika njia ambazo hawazijui. Mbele yao nitaligeuza giza kuwa mwangaza, na pahali penye kuharibika patakuwa laini. Huo ndio mupango wangu wa kufanya, nami nitautimiza.
Halafu miti yote katika inchi itajua kwamba mimi Yawe ninaishusha miti mirefu na kuinua miti mifupi. Mimi ninakausha miti mibichi na kustawisha miti yenye kukauka. Ni mimi Yawe ninayesema hayo na nitayafanya.