Luka 3:23 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 200223-38 Wakati Yesu alipoanza kazi yake alikuwa na umri wa miaka yapata makumi tatu. Yeye alizaniwa kuwa mwana wa Yosefu. Yosefu alikuwa mwana wa Heli, Heli alikuwa mwana wa Matati, Matati alikuwa mwana wa Lawi, Lawi alikuwa mwana wa Melki, Melki alikuwa mwana wa Yana, Yana alikuwa mwana wa Yosefu, Yosefu alikuwa mwana wa Matatia, Matatia alikuwa mwana wa Amosi, Amosi alikuwa mwana wa Nahumu, Nahumu alikuwa mwana wa Esili, Esili alikuwa mwana wa Nage, Nage alikuwa mwana wa Mati, Mati alikuwa mwana wa Matatia, Matatia alikuwa mwana wa Simei, Simei alikuwa mwana wa Yosefu, Yosefu alikuwa mwana wa Yoda, Yoda alikuwa mwana wa Yoana, Yoana alikuwa mwana wa Resa, Resa alikuwa mwana wa Zerubabeli, Zerubali alikuwa mwana wa Saltieli, Saltieli alikuwa mwana wa Neri, Neri alikuwa mwana wa Melki, Melki alikuwa mwana wa Adi, Adi alikuwa mwana wa Kosamu, Kosamu alikuwa mwana wa Elmadamu, Elmadamu alikuwa mwana wa Eri, Eri alikuwa mwana wa Yoshua, Yoshua alikuwa mwana wa Eliezeri, Eliezeri alikuwa mwana wa Yorimu, Yorimu alikuwa mwana wa Matati, Matati alikuwa mwana wa Lawi, Lawi alikuwa mwana wa Simeoni, Simeoni alikuwa mwana wa Yuda, Yuda alikuwa mwana wa Yosefu, Yosefu alikuwa mwana wa Yonamu, Yonamu alikuwa mwana wa Eliakimu, Eliakimu alikuwa mwana wa Melea, Melea alikuwa mwana wa Mena, Mena alikuwa mwana wa Matata, Matata alikuwa mwana wa Natani, Natani alikuwa mwana wa Daudi, Daudi alikuwa mwana wa Yese, Yese alikuwa mwana wa Obedi, Obedi alikuwa mwana wa Boazi, Boazi alikuwa mwana wa Salmoni, Salmoni alikuwa mwana wa Nasoni, Nasoni alikuwa mwana wa Aminadabu, Aminadabu alikuwa mwana wa Aramu, Aramu alikuwa mwana wa Hesironi, Hesironi alikuwa mwana wa Peresi, Peresi alikuwa mwana wa Yuda, Yuda alikuwa mwana wa Yakobo, Yakobo alikuwa mwana wa Isaka, Isaka alikuwa mwana wa Abrahamu, Abrahamu alikuwa mwana wa Tera, Tera alikuwa mwana wa Nahori, Nahori alikuwa mwana wa Serugu, Serugu alikuwa mwana wa Reu, Reu alikuwa mwana wa Pelegi, Pelegi alikuwa mwana wa Eberi, Eberi alikuwa mwana wa Sela, Sela alikuwa mwana wa Kainana, Kainana alikuwa mwana wa Aripakisadi, Aripakisadi alikuwa mwana wa Semu, Semu alikuwa mwana wa Noa, Noa alikuwa mwana wa Lameki, Lameki alikuwa mwana wa Metusela, Metusela alikuwa mwana wa Enoki, Enoki alikuwa mwana wa Yaredi, Yaredi alikuwa mwana wa Mahaleli, Mahaleli alikuwa mwana wa Kainana, Kainana alikuwa mwana wa Enosi, Enosi alikuwa mwana wa Seti, Seti alikuwa mwana wa Adamu, Adamu aliumbwa na Mungu. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Haya ni majina ya babu za Yesu Kristo, wa uzao wa Daudi, wa uzao wa Abrahamu. Abrahamu alizaa Isaka, Isaka alizaa Yakobo, Yakobo alizaa Yuda na wandugu zake, Yuda alizaa Peresi na Zera kutoka muke wake Tamari, Peresi alizaa Hesironi, Hesironi alizaa Ramu, Ramu alizaa Aminadabu, Aminadabu alizaa Nasoni, Nasoni alizaa Salmoni, Salmoni alizaa Boazi kutoka muke wake Rahaba, Boazi alizaa Obedi kutoka muke wake Ruta, Obedi alizaa Yese, Yese alizaa mufalme Daudi, Daudi alizaa Solomono (mama yake ndiye yule aliyekuwa muke wa marehemu Uria), Solomono alizaa Rehoboamu, Rehoboamu alizaa Abiya, Abiya alizaa Asa, Asa alizaa Yosafati, Yosafati alizaa Yoramu, Yoramu alizaa Uzia, Uzia alizaa Yotamu, Yotamu alizaa Ahazi, Ahazi alizaa Hezekia, Hezekia alizaa Manase, Manase alizaa Amoni, Amoni alizaa Yosia, Yosia alizaa Yekonia na wandugu zake, wakati Waisraeli walipohamishwa kwenda Babeli. Nyuma ya kuhamishwa kwa Waisraeli kwenda Babeli, Yekonia alizaa Saltieli, Saltieli alizaa Zerubabeli, Zerubabeli alizaa Abihudi, Abihudi alizaa Eliakimu, Eliakimu alizaa Azoro, Azoro alizaa Zadoki, Zadoki alizaa Akimu, Akimu alizaa Elihudi, Elihudi alizaa Eleazari, Eleazari alizaa Matani, Matani alizaa Yakobo, Yakobo alizaa Yosefu, yule alikuwa mume wa Maria, mama ya Yesu, anayeitwa Kristo.